Blog Archives
TUZIBEBE KANGA ZETU
TUZIBEBE KANGA ZETU
Leo siku ya simanzi
tuzibebe kanga zetu.
Tusambaze kona zake nne
zikawe ngao ya uchungu wetu.
Kanga zetu zibebe faraja
hadharani na faraghani.
Magufuli katutoka
kama jua linalozama.
Tuzibebe kanga zetu
tukasambaze matumaini.
Machozi yatutiririka
kwa kasi ya mto Ruvu.
Tuzibebe kanga zetu
tukadeki nyuso zetu.
Kilio kimetutia kikwi
tujisitiri na kanga zetu.
Waliotangulia tuwaombee
heri iwavushe kwa maulana.
Tuzibebe kanga zetu
kama mkeka wa sala.
Kanga zetu tuzifukize rehema
ili tujawe karama.
Vinyongo na visasi tupepee
vitoweke kwa haya na soni.
Marehemu wetu tuwaenzi
fedheha sio kanga yetu.
Tuilinde amani yetu
kwa umaridadi wa kanga.
Tuyavae maneno mema
kwa madaha ya utanashati.
Tuzibebe kanga zetu
tukamuage baba yetu.
Tamati ya maisha imefika
buriani haitoshi pindo.
Kanga zetu ni vigawanyio
kati ya mauti na maisha.
Sare za kanga zetu
ni shada zenye thamani.
Tutandike kanga zetu
kwenye njia ya mazishi.
Waliolala wanafarijika
kusindikizwa kifahari.
Tuzibebe kanga zetu
safari ya baba imekwisha.
Translation/Subtitles:
LET US CARRY OUR KANGAS
Today is a day of mourning
let us carry our kangas.
Let us spread its four corners
as a shield for our pain.
Our wraps should carry comfort
publicly and privately.
Magufuli has left us
like the setting sun.
Let us carry our kangas
to go spread hope.
Tears are welled up
like the speed of the Ruvu river.
Let us carry our kangas
to mop our faces.
Weeping has hiccupped us
let us shield ourselves with our kangas.
Let us pray for the gone ones
to cross over with blessings.
Let us carry our kangas
like a prayer mat.
Let us fragrance our kangas with mercy
so we may be gifted with deliverance.
Let us wave away bitterness and vengeance
that they depart ashamed and confounded.
Let us honour our late loved ones
for ridicule is not our kanga.
Let us protect our peace
with beauty of the wrap.
Let us wear good words
with pride of elegance.
Let us carry our kangas
to bid farewell to our father.
The end of life has come
farewell does not fit the hem.
Our kangas are a border
between death and life.
Our kangas as uniforms
are valuable wreaths.
Let us lay our kangas
on the road to the funeral.
Those gone are comforted
by this elegant escort.
Let us carry our kangas
our father’s journey is over.